Jumatano , 14th Sep , 2022

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Maria Basso mwenye umri wa miaka 20, anadaiwa kuuawa katika tukio la uvamizi lililofanywa na vijana zaidi ya 30 wanaodhaniwa kuwa ni panya road huku wengine wawili wakijeruhiwa.

Maria Basso, aliyeuawa na panya road

Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2022, eneo la Kawe Mzimuni jijini Dar es Salaam, ambapo vijana hao pia wamepora vitu mbalimbali ikiwemo simu na fedha.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea huku mama mzazi wa Maria anayedaiwa ameeleza kusikitishwa kwake kwa vijana hao kutochukuliwa hatua na kukamatwa kwa kuwa wameendelea kuleta taharuki kwa wananchi.

Aidha marehemu Maria Basso (24) alikuwa ni mwanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma - UDSM.