Jumatano , 28th Jan , 2015

Mtayarishaji muziki Mr T Touch amesema kuwa kwa mwaka huu mpya, amejikita katika kuhakikisha kuwa kazi zote anazofanya zinakuwa katika kiwango na zinaleta mchango wa kipekee katika jamii.

Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania Mr T - Touch akiwa na Ney na Sheddy

Mr T amesema haya wakati akijitetea kutokana na tuhuma za kumnyang'anya msanii chipukizi Daddy Beda mdundo aliomtengenezea na kumpa msanii Darasa, kitendo ambacho amejitetea kukifanya baada ya kuona mdundo huo umemzidi uwezo chipukizi huyo.