Ijumaa , 2nd Sep , 2022

Benki ya CRDB imeingia ushirikiano na taasisi ya Selcom ambao utasaidia kurahisisha huduma za malipo kupitia simbanking  kwa wateja wanaotumia benki hiyo 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es salaam Afisa mwendeshaji mkuu wa benki ya CRDB Bruce Mwile amesema kupitia ushirikiano huo wateja wao watakuwa wamewarahisishia huduma za malipo  na popote watakapokuwepo na kuona huduma za selcom ni sawa na wakala wa CRDB hivyo anaweza kufanya malipo

Kwa upande wake mkurugenzi wa wateja wa awali na wa kati CRDB Benki Bonaventura Paul amesema mpango huo pia utasaidia kupunguza tabia za baadhi ya wateja kutoa fedha na kutembea nazo mifukoni na kufahamu pia aina za huduma ambazo wateja wa CRDB wanapenda kuzitumia

Naye mkuu wa kitengo cha biashara selcom Godfrey Mwakamnyanda amesema wameamua kuingia mashirikiano hayo kutokana na kutambua ukubwa wa benki ya CRDB hapa nchini katika utoaji wa huduma zaje Kwa watanzania