Alhamisi , 14th Jul , 2022

Kiongozi wa mbio za mwenge Sahili Geraruma amewataka viongozi watakaochaguliwa kuchukua taarifa za watu katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 ya mwezi ujao kutotumia vibaya taarifa hizo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

Geraruma ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza na kuwatoa hofu wananchi kwa kuwataka kutoa taarifa zao katika zoezi hilo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kali amesema mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa kilometa 120 za wilaya hiyo na kukagua miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3.