Mkuu wa Idara ya Michezo East Africa TV na East Africa Radio, David Kampista (kushoto) akipokea mchango wa taulo za kike kutoka kwa Melkczedeck Bruno.
Bruno anasema wakati kampeni hii inaanza mwaka 2017 alikuwa bado kijana mdogo, alitamani kushiriki kuchangia lakini hakuweza. Mwaka huu alijipanga na ametimza ahadi yake ya kusaidia wanafunzi wa kike mashuleni.
Kwa pamoja tunaweza kutokomeza sifuri kwa watoto wa kike mashuleni kwa kutengeneza mikakati dhidi yao na kuwapa elimu ya kutosha.