Jumatatu , 20th Jun , 2022

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde ameupongeza mkoa wa Mbeya chini ya uongozi wa Mkuu wa mkoa huo Juma Homera, kwa kuchukua hatua ya uanzishwaji wa mashamba makubwa (block farms) ambayo ni maalum kwa ajili ya kilimo cha Maharage ya Soya.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema wilayani Chunya alipotembelea na kukagua mashamba hayo na kufanya mikutano ya wananchi katika Kata za Nkung’ungu na Lupa zilizopo Tarafa ya Kipembawe,Chunya.

"Niwapongeze sana mkoa wa Mbeya chini ya uongozi wa RC Homera kwa utayari wenu wa kutenga ekari 100,000 za kilimo cha Soya ili kuchangamkia fursa hii iliyoletwa na kampuni ya Longping High Tech ambao pamoja na huduma nyingine za kitaalamu pia wataleta mbegu bora, teknolojia bora na watakuwa soko la mazao ya wakulima," amesema Naibu Waziri Mabunde

"Mkakati wa Wizara ni kuwa na mashamba makubwa 10,000 kama haya ifikapo mwaka 2030 katika kuelekea kuikuza sekta ya kilimo asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, hii ni fursa kubwa ya vijana wengi kushiriki kwenye kilimo ili malengo haya ya nchi yaweze kutimia,"ameongeza.