Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa.
Ratiba ya mihula ya kufunga na kufungua vyuo ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu mwaka huu, imeibua hofu kwa wasomi wa vyuo mbalimbali nchini kutoshiriki ipasavyo kwenye uchaguzi mkuu ujao, ambapo jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) mkoani Mbeya wamelibaini hilo na kuanza kupaza sauti zao kuidai haki hiyo
Kutokana na hofu hiyo, CHASO imeandika waraka na kuuelekeza katika ofisi ya katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo ikimtaka kuwatumia wabunge wake kupeleka hoja binafsi bungeni ya kurekebisha sheria ya uchaguzi ili iwaruhusu watanzania wote kupiga kura wakiwa mahali popote ndani ya mipaka ya Tanzania.
Baadhi ya wanafunzi hao pia wakaelezea umuhimu wa wao kupiga kura, huku wakidai kuwa hawako tayari kunyimwa haki yao ya kikatiba kwenye uchaguzi mkuu ujao