Jumanne , 19th Apr , 2022

Unaambiwa mwanamke anayefahamika kwa jina la Carrie mwenye miaka 53 kutoka Colorado USA, ameshangaza watu kwa kunywa mkojo wake kwa miaka minne sasa.

Picha ya Carrie akinywa mkojo wake

Mwanamke huyo alianza kunywa glasi moja kwa siku lakini sasa hivi anakunywa glasi tano za mkojo wake kwa siku sawa na lita 2.3.

Carrie amesema mkojo wake unanuka pia una ladha ya chumvi au champagne na ladha nyingine tofauti ambayo hutegemea na kitu anachokula, pia ni rahisi kwake kunywa mkojo kuliko maji.

Aidha ameongeza kusema hutumia mkojo wake kupiga mswaki kwa sababu huifanya meno yake kuwa meupe.

Chanzo : DMax.