Jumamosi , 19th Apr , 2025

Aliyewahi kuwa mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania kupitia Lino Angency International Ltd, Hashim Lundenga, amefariki dunia Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Hashim Lundenga

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndie aliyesimamia kwa mafanikio makubwa mashindano haya ya urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mkubwa.

Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.