Jumatano , 23rd Apr , 2025

Kuelekea mchezo wa fainali Copa del Rey tarehe 26/Aprili, Kocha Carlo Ancelotti amesema ili Madrid wawe mabingwa wa Copa del Rey na La Liga wanapaswa kuwafunga FC Barcelona.

Kocha Carlo Ancelotti

Timu hizo mbili zitakutana hatua ya fainali kwenye Kombe hilo Jumamosi hii huku katika msimamo wa La Liga wakitofautiana alama 4.

"Ikiwa tunataka kushinda Copa del Rey na La Liga lazima tushinde dhidi ya Barca, hii ni wazi. Hakuna shaka. Natamani kusalia Real Madrid, hii bado ni HONEYMOON, nina furaha sana. Presha nyingi, kweli, tunakaribia mwisho wa msimu".-Kocha  Carlo Ancelotti

Carlo Ancelotti amethibitisha pia kuwa Kylian Mbappé amerejea kwenye mazoezi ya timu leo ​ tayari kwa fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barca!