
kikosi cha Yanga.
Gindi pia amasema kuwa uwepo wa kikosi cha Yanga kwenye mkoa huo ni fursa kwa wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na pia wafanyabiashara wa chakula kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya mashabiki wanataokwenda kushuhudia mchezo.
“Yanga ni timu kubwa na popote pale inapocheza inatoa fursa kubwa kwa wakazi wa maeneo husika, hivyo kwa kweli tunawashukuru viongozi wa Ruvu Shooting kwa kutuletea mchezo huu hapa mkoani kwetu,” amesema Omari Gindi.
Uongozi wa Ruvu umetumia kanuni ya 9 kifungu cha (7) inayoruhusu klabu kuhamisha mechi zao mbili za nyumbani kwenye viwanja visivyokuwa na mechi za Ligi Kuu.
Mara ya mwisho kwa Yanga kucheza kwenye uwanja huo ilikuwa Julai 25, mwaka jana ilipofungwa bao 1 kwa 0 na Simba katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na katika mchezo wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Ruvu ambapo Yanga ilishinda mabao 3-1.