Jumamosi , 16th Apr , 2022

Shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Amnesty International UK, limeikosoa hatua ya Uingereza ya mpango wake wa kutaka kuwahamisha wakimbizi kutoka Nchini humo na kuwapeleka nchini Rwanda, ikionekana ni kufanya biashara ya kuuza watu jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.

Moja ya Kambi ya wakimbizi ya Shirika la Kimataifa la kuhudumia Wakimbizi, UNHCR

Mkurugenzi wa Amnesty International UK, Steve Valdez-Symonds amesema kitendo hicho sio ubinadamu, na kwamba Mpango huo hautapunguza idadi ya wakimbizi bali utasababisha kiasi kikubwa cha ukatili na kuchochea njia hatari zaidi za wakimbizi kuanzishwa.

Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda kuhusu maamuzi hayo, ikielezwa kwamba yatawahusu watu wote wanaoingia Uingereza kinyume cha Sheria.