Jumamosi , 16th Apr , 2022

Takribani Wapalestina 152 wamejeruhiwa jana Ijumaa baada ya kuzuka mapambano kati ya vikosi vya usalama vya Israel na Wapalestina katika eneo takatifu la msikiti al-Aqsa mjini Jerusalem. 

Hizi ni vurugu kubwa za hivi karibuni, ambazo zinazusha mashaka ya huenda eneo hilo likarejea katika mgogoro mkubwa. 

Shirika la msalaba mwekundu limesema idadi kubwa ya Wapalestina waliojeruhiwa ilitokana na ufyatuaji wa risasi za mpira, mabomu ya machozi pamoja na kuchapwa bakora.

Maelfu ya Waislamu walitarajiwa katika mji huo wa kale wa Jerusalem kuswali katika eneo hilo la msikiti wa al-Aqsa Ijumaa, wakati huu wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan. 

Kufuatia vurugu hizo, kupitia ukurasa wake wa Twitter, msemaji wa ofisi Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennet amesema polisi iliwashikilia mamia ya Wapalestina 

Mzozo wa Israeli na Palestina umeeendelea kukua katika siku za hivi karibuni , baada ya mashambulizi mabaya kutokea nchini Israel yakihusisha raia wa Palestina.

Zaidi ya Wapalestina 20 ambao walikua na silaha wameuawa  tangu Israel ianze kuchukua hatua ya kukomesha mashambulizi hayo huko   West Bank,  kwenye wilaya ya  Jenin