Jumamosi , 16th Apr , 2022

Ikiwa ni siku chache baada ya kuzuru Ukraine na kuzungumza na Rais wa Ukraine, Urusi imetangaza kumzuia Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuingia nchini humo kutokana na msimamo wake wa uhasama kuhusu vita vya Ukraine.

Wazari Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alipoitembelea Ukraine

Akitoa taarifa hiyo leo Aprili 16, 2022, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Liz Truss amesema kuwa Waziri Mkuu wa zamani Theresa May na waziri wa kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon ni miongoni mwa raia wa Uingereza na wanasiasa kadhaa waliozuiwa kuingia nchini Urusi.

Hatua hii imechukuliwa kwa kuzingatia hatua ya uhasama isiyo isiyo ya kawaida ya Serikali ya Uingereza, hasusani kuweka vikwazo dhidi ya Maaafisa Wakuu wa Urusi na kusema Urusi itaongeza orodha hiyo hivi karibuni.

Hadi sasa, tayari Urusi imemzuia Rais wa Marekani Joe Biden na maafisa wengine wengi wa Marekani kuingia nchini humo tangu vita yake na Ukraine ilipoanza.