
(Nyota wa Simba Shomari Kapombe akishangilia goli kwenye mchezo dhidi ya Asec Mimosas)
“Sisi tulijiandaa na mpinzani yoyote baada ya kuingia hatua ya robo fainali na kupambana na timu kama Orlando, sisi kama wachezaji tumefurahia mana kama sisi wachezaji tunapenda kucheza mechi kubwa na hii ni mechi kubwa na inatuonyesha kama Simba tumefikia katika sehemu gani kwenye mashindano haya “amesema Kapombe
Huku kocha mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco akiwataka mashabiki wa klabu ya Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Orlando Pirates huku akisema mchezo huo ni muhimu sio kwa Simba tu bali hata kwa ajili ya taifa
“Akili zote zipo kwa ajili ya mchezo wa kesho ,tunakwenda kufanya kila kitu kwa ajili ya nchi,timu na mtu mmoja mmoja maana huu ni wakati wetu na kesho ndio itatupa picha kama tunakwenda kuweka historia au ndio itakuwa mwisho wa safari ,lakini lengo letu la kucheza ligi ya mabingwa bado ipo palepale hususani kufika hatua ya makundi na kufika mbali na kesho tunakwenda kufanya kile ambacho nyuma huwa tunafanya pia “amesema Pablo