
Bw. Frank James, mwenye umri wa miaka 62, alipelekwa mahakamani siku ya jana kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi kwenye halaiki kubwa ya watu.
Alitiwa mbaroni baada ya msako mkali na polisi ambapo idadi ya watu walioumia kwenye tukio hilo imefikia watu 23.
Mtuhumiwa huyo hajakana mashtaka yake, Lakini Mwanasheria wake ameomba mahakama ipate ripoti ya mtaalamu wa magonjwa ya akili.
Mwanasheria Breon Pearce akisoma hati ya mashataka alisema ‘’Mtuhumiwa alifanya shambulizi kwa wana New Yorke majira ya asubuhi kwenye kituo cha treni’’
Endapo atakutwa na hatia, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Anatuhumiwa kuwapiga risasi watu 10 na kuwaua wengine 13, ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia huku akisahau vitambulisho muhimu ikiwemo kadi ya benki ambayo ilikua na jina lake.
Pia alikutwa na silaha ambayo ilinunuliwa kihalali huko Ohio imesajiliwa kwa jina "Frank Robert James".