Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Tenis, Khalid Msemo amesema mchezo huo umekuwa na wachezaji wengi kutoka nje ya nchi hususani kwa wasichana suala linalopelekea kushindwa kuwa na vijana wengi watakaoweza kushiriki mashindano mbalimbali makubwa ya ndani na nje ya nchi.
Msemo amesema, wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha vijana kupenda na kushiriki katika michezo ili kuwajenga kielimu na kiafya.
Msemo amesema, mpaka sasa Tanzania imekuwa na vijana wengi wanaoshiriki mchezo huo waishio nje ya nchi na sio waishio hapa Tanzania tofauti na nchi za wenzetu ambapo wana vijana wengi ambao wanashiriki mchezo huu.
Msemo amesema, kama jamii itashiriki katika kuhamasisha watoto kushiriki katika mchezo huo, anaamini Tanzania itakuwa na vijana wengi na wenye uwezo wa kushiriki mashindano makubwa na kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.