Jumanne , 12th Apr , 2022

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere amewasilisha bungeni ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 na kutoa hati 999 za ukaguzi katika maeneo mbalimbali.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere

Akitoa taarifa ya ripoti hiyo mbele ya wanahabari CAG Charles Kichere amebainisha kuwa alipopita katika taarifa za fedha za NHIF, amebaini kuwa wanaume wamepewa huduma ya kujifungua kwenye vituo vya afya.

Aidha CAG amesema kati ya hati 999 zilizotolewa 185 za mamlaka zaserikali za mitaa 195 mashirika ya umma na 308 za serikali kuu.

CAG Kichere akizungumzia ukaguzi kwa upande wa vyama vya siasa amesema kati vya vyama tisa vilivyokaguliwa vinne vina hati mbaya vikiwamo Chauma na TLP.

Akizungumzia kuhusiana na ukaguzi maalum 56 uliofanyika mwaka 2021 mamlaka ya serikali za mitaa inaongoza kwa kaguzi 37 serikali kuu 12 na mashirika ya umma 6.