Jumanne , 12th Apr , 2022

Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa Takribani watu 30 wameuawa katika mapigano yaliyodumu kwa siku mbili na watu wenye silaha huko mashariki  mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la Ituri jirani na Kivu ya kaskazini, ingawa maeneo hayo yapo chini ya mamlaka za serikali kujaribu kuzuia mashambulizi ya watu wenye silaha. 

Mashambulizi hayo yanasemekana kufanywa na kundi la waaasi la Allied Democratic Front (ADF),kundi linalosemekana kuwa hatari sana kwenye ukanda huo.

 
Kundi hilo linasemekana kufanya mauaji ya kikatili, ambapo baadhi ya watu walikutwa wamefungwa mikono na kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni, huku nyumba za wakazi zikichomwa moto na mali kuibiwa 
Mwezi December mwaka jana zaidi ya askari 1,000 wa Uganda walipelekwa nchini  DR Congo ili kujaribu kuzuia mashambulizi hayo kutoka kwa waasi wa kundi   ADF.

Lakini licha ya juhudi hizo, bado kumekua na mashambulizi makali kutoka kwenye kundi hilo ambalo hushambulia jamii. 

Kaskazini mwa Kivu kundi lingine la waasi liitwalo M23 limeendelea na mauaji na kusababisha hali ya usalama kuwa tete zaidi.