Alhamisi , 7th Apr , 2022

Nyota wa Real Madrid Mfaransa Karim Benzema ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat tric dhidi ya klabu ya Chelsea kwenye michuano ya ulaya kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

(Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema)

Benzema alifunga magoli hayo mnamo dakika ya 21,24 na 46 huku ikiwa ni hat tric yake ya pili mfululizo baada ya kuwafunga klabu ya Paris Saint Germain(PSG) kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora na sasa ameifikia rekodi ya nyota watatu ambao waliiweka hapo kabla ambao ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi msimu wa 2016/17 sambamba na Luiz Adriano mnamo msimu wa 2014/15

“Huu ni miongoni mwa usiku za maajabu kama ilivyokuwa kwenye dimba la Bernabeu dhidi ya PSG,leo tulikuja hapa kushinda na tumeonesha sisi ni Real Madrid.Mipango yetu imekwenda vizuri kama tulivyopanga na kucheza kutokea dakika ya kwanza mpaka ya mwisho katika mipango yetu  “amesema Benzema

Benzema sasa amefikisha magoli 37 kwenye michezo 36 aliyoicheza kwenye mashindano yote ya msimu huu, huku sasa akifikisha jumla ya magoli 82 kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa nyuma ya magoli 3 ya mshambuliaji Robert Lewandowski wa Bayern Munich  anayekamata nafasi ya tatu kwa ufungaji wa muda wote kwenye Uefa champions league