JKU waliitoa Yanga katika mchezo wa Robo fainali baada ya kufunga bao 1-0 katika Dakika ya 72, Mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mtibwa Sugar nao waliitoa Azam FC kwa mikwaju ya Penati 7-6 baada ya Mechi yao kumalizika kwa bao 1-1 ndani ya dakika 90.
Nusu Fainali nyingine itakayopigwa hapo kesho, itawakutanisha Polisi ya Zanzibar na Simba SC uwanja wa Amaan, Zanzibar ambapo Polisi waliwafunga Mabingwa watetezi wa Kombe hilo KCCA kwa mikwaju ya Penati 5-4 baada ya kumaliza Dakika 90 na kutoshana nguvu kwa bao 0-0.
Simba iliibwaga Taifa ya Jang'ombe kwa bao 4-0 hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya Nusu fainali ambapo Fainali inatarajiwa kufanyika Januari 13 Uwanja wa Amaan visiwani humo kwa kuzikutanisha Mshindi kati katika mechi ya JKU na Mtibwa Sugar na Mechi kati ya Polisi na Simba SC.