Ijumaa , 18th Mar , 2022

Droo ya ligi ya mabingwa barani ulaya (Uefa champions league ) kwa hatua za robo na nusu fainali zimepangwa leo mjini Nyon nchini Uswizi huku michezo ya mkondo wa kwanza na wa pili kwa hatua ya robo fainali ikitarajiwa kuchezwa mnamo april 5 na 6.

(Michezo ya robo fainali ligi ya mabingwa ulaya)

Na baada ya muchezo ya mkondo ya kwanza, michezo ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa mnamo April 12 na 13. 2022.

Kwenye droo hiyo mabingwa watetezi wa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya (uefa champions league) Chelsea wamepangiwa kucheza na mabingwa mara 13 wa Uefa Real Madrid los blanco kwenye hatua ya robo fainali ambapo mshindi atakutana na mshindi baina ya Manchester city au Atletico Madrid kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Ikumbukwe katika historia ya Real madrid hawajawahi kuifunga Chelsea katika michezo ya kimashindano.

Nao Majogoo wa meserside Liverpool wamepangiwa kucheza na Benfica ya Ureno kwenye hatua hiyo wakati kwenye hatua ya nusu fainali watapambana na mshindi kati ya klabu ya Bayern munich au Villareal watakao pambana kwenye hatua nya robo fainali.