Jumatatu , 29th Dec , 2014

Msanii maarufu wa filamu nchini, Irene Uwoya ameweka wazi kuhusiana na filamu ambazo zimemuinua na kuweza kuliteka soko la filamu ndani na nje ya nchi kwa mwaka huu wa 2014.

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Irene Uwoya

Irene ameelezea kuwa filamu ambazo zimempa kipaumbele na kuweza kufanya kazi nje ya nchi zikiwemo 'Who is My Child', Shameless Family na 'Kitoga', ambazo zote ziko sokoni zikiendelea kumng'arisha na hivi sasa akijiandaa kutoa kazi kwa ajili ya kuufungua mwaka mpya.

Aidha, Irene ameelezea kuwa pamoja na ushiriki wake katika kazi za uigizaji ameishukuru kampuni ya 5 Effect Movies ambayo imempa sapoti kubwa ambapo kwa sasa wamejiandaa kutoa kazi mpya za kuufungua mwaka mpya.