Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa
Kufuatia hali hiyo, serikali inafanya juhudi za haraka kulirudisha eneo ilo lenye kilometa kwa wananchi ili kuepusha mgogoro unaohatarisha usalama wa wananchi wanaonyanyaswa na askari wa wanyamapori bila sababu ya msingi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa ametoa kauli hiyo baada ya kumalizika kwa ziara ya Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira iliyotembelea maeneo yenye migogoro kati ya hifadhi za taifa mapori ya akiba na wananchi amesema kuwa eneo ilo halipo katika ramani ya pori la akiba la Mkungunero hivyo hakuna sababu ya wananchi kunyanyaswa katika ardhi yao.
Awali wakitoa malalamiko ya kwa kamati hiyo wakazi wa kijiji hicho wamesema matendo wanayofanyiwa na askari wa pori hilo si ya kibinadamu huku wakidai kuwa hawajawahi kukaa na kubariki eneo ilo kuwa sehemu ya pori lakini wanapigwa na kujeruhiwa wanapoingiza mifugo.
Naye mbunge wa Kiteto Benedikto Ole Nangoro aliiomba wizara kuangalia kwa kina sulala hilo ombi ambalo imesikika.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira James Lembeli aliwataka wakazi hao kuwa watulivu kwakuwa kamati yake itamaliza kero hiyo ambayo sasa imemalizika kwa serikali kutoa tamko la kuzirudisha kilometa hizo 50 kwa wananchi.