Jumatano , 24th Dec , 2014

Bondia Iddy Bonge na Mussa Mbabe wanatarajia kupanda ulingoni kesho, katika pambano la uzito wa juu la Raundi nane la kumaliza ubishi litakalofanyika ukumbi wa Friends Corner Manzese, jijini Dar es salaam.

Bondia Mussa Mbabe

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST, Anthony Rutta amesema pambano hilo litatanguliwa na mapambano 17 kutoka kwa mabondia mbalimbali chipukizi katika mchezo huo.

Rutta amesema pambano hilo, litakuwa la kufunga mwaka kwa upande wa PST ambapo wataanza maandalizi kwa ajili ya mapambano mengine mwakani ikiwa ni sehemu ya kukuza na kuutangaza mchezo huo hapa nchini.

Kwa upande wake, Bondia Mussa Mbabe amesema anaamini atashinda pambano hilo kutokana na mazoezi ya muda mrefu aliyoyafanya kwa ajili ya pambano hilo na hatokubali kushindwa kwani anauelewa na mpinzani wake.

Kwa upande wake, Iddy Bonge amesema hatokubali kupingwa na Mbabe kutokana na mazoezi na uzoefu alionao katika mchezo huo.