Jumapili , 21st Dec , 2014

Kocha wa Timu ya Tenisi ya walemavu, Riziki Salum amesema wameamua kufanya mashindano ya kufunga mwaka kwa vijana wakiwa na lengo la kukuza vipaji vya vijana hao.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo, Riziki amesema wameamua kuandaa mashindano hayo kutokana na Chama ambacho ndio wahusika kutojihusisha na suala lolote kuhusiana na kukuza vipaji vya walemavu.

Riziki amesema katika mwaka huu, vijana wamefanya vizuri katika michuano mbalimbali waliyoshiriki ya ndani na nje ya nchi kutokana na maandalizi yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wa timu.