Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Job Ndugai
Akizungumzia migogoro hiyo ambayo imeonekana kushika kasi katika Wilaya za Kiteto mkoani Manyara na Kilosa mkoani Morogoro, Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema wao kama serikali wanatakiwa kutoa elimu ya kutosha hasa katika maeneo yenye migogoro ya mara kwa mara.
Aidha Mh. Ndungai amebainisha kuwa mbali na kugombea ardhi baadhi ya makundi ya jamii za wakulima na wafugaji wameonekana kukosa imani ya dini jambo linalowafanya kutokuwa na hofu ya kumwaga damu, hivyo kuomba viongozi wa dini nao kuongeza huduma za kiroho katika maeneo hayo.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata habibu simbamkuti amesema swala la migogoro ya ardhi ni tatizo la muda mrefu na linaonekana kuchangiwa zaidi na serikali kwa kushindwa kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji, na kwamba migogoro hiyo haitaweza kwisha kama serikali haitachukua jitihada za makusudi kupima na kutenganisha maeneo ama wakulima na wafugaji kuungana ili kuishinikiza serikali kuwaonyesha maeneo yao badala ya kugombana wenyewe kwa wenyewe.