Ijumaa , 6th Aug , 2021

Timu ya taifa ya Mexico ya vijana chini ya umri wa miaka 23 imefanikiwa kushinda medali ya shaba baada ya kuwafunga timu wenyeji, timu ya taifa ya Japan kwa mabao matatu kwa moja na kuibuka kuwa washindi watatu wa michuano ya Olympic kwa upande wa soka la wanaume.

Timu ya Mexico ikishangilia kwa kumrusha juu kocha wake, Jaime Lozano baada ya kuibuka kuwa washindi watatu wa Olympic kwa upande wa soka na kupata medali ya shaba mchana wa leo kwa kuifunga Japana 3-1.

Sebastian Cordova ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia bao Mexico dakika ya 13, Johan Vasquez alizidi kuwapa uongozi Mexixco baada ya kufunga bao la pili dakika ya 22 kabla ya Alexis Vega kufunga bao la tatu dakika 58 ilhali Kaoru Mitoma alifunga bao la kufutia machozi kwa upande wa Japan dakika ya 78 kwenye mchezo uliochezwa mchana wa leo Agosti 6, 2021 kwenye uwanja wa Saitama nchini Japan.

Ushindi huo umeifanya Mexico kupata medali ya pili ya Olympic kwa upande wa soka baada ya wababe hao kutoka Amerika kaskazini na kati kubeba medali ya dhahabu ya Olympic kwa kuwa  mabingwa mwaka 2016 kwenye mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil.

Baada ya mshindi watatu kupatikana, mchezo wa fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani unatazamiwa kuchezwa saa 11:30 jioni ya kesho Agosti 7, 2021 ambapo mabingwa watetezi Brazili watacheza na mabingwa wa mwaka 1992, timu ya taifa ya Hispania kwenye uwanja wa New National Arena uliopo nchini Japan.