Ijumaa , 6th Aug , 2021

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, na wenzake imeahirishwa hadi Agosti 13, 2021, baada ya upande wa serikali kudai kwamba taratibu za kufungua kesi ya ugaidi katika Mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza bado hazijakamilika. 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA na wenzake walifikishwa Mahakamani mapema leo Agosti 6, 2021, baada ya hapo jana kesi hiyo kushindwa kuendeshwa kufuatia matatizo ya kimtandao yaliyohusisha usikilizaji kesi kwa video conference baina ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Gereza la Ukonga.