
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kagera ambapo alitembelea ofisi za TTCL na Shirika la Posta Tanzania (TPC) na kuona kuwa Meneja wa TTCL mkoani humo hatoshi kuwa katika nafasi hiyo ukizingatia Kagera ni mkoa wa kimkakati kwa sababu unapakana na nchi takribani nne hivyo Meneja wake anatakiwa kuwa na uwajibikaji wenye ufanisi mkubwa.
"Ninaagiza Meneja wa mkoa wa Kagera aondoshwe mara moja na kuanzia leo asitambulike kama Meneja wa mkoa wa Kagera, taratibu zifuatwe na apangiwe kazi zingine kulingana na wasifu wake kitaaluma ili aweze kufanya kazi vizuri kwa sababu majukumu ya sasa hana uwezo nayo," amesema Mhandisi Kundo.