Ijumaa , 25th Jun , 2021

Klabu ya soka ya Manchester City imethibitisha kupeleka ofa ya Pauni Milioni 100 sawa na Bilioni 300 kwa fedha ya Kitanzania katika timu ya Aston Villa kwa ajili ya kumnasa kiungo mchezeshaji Jacky Grealish ikiwa ni rekodi ya uhamisho kwa Ligi kuu ya England.

Jack Grealish

Kocha Pep Guardiola licha yakuwa bingwa msimu huu, na pia kucheza fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Chelsea, ambapo alipoteza kwa bao 1-0 inaonekana kuhitaji zaidi kuboresha kikosi chake.

Guardiola amekusudia kufanya usajili wa kutisha katika kikosi chake kwa msimu ujao,licha ya Jack Grealish, pia anakusudia kumpata Harry Kane kutoka Tottenham kuziba nafasi ya Sergio Kun Aguero aliyetimkia Barcelona.

Jack Grealish yupo katika kiwango bora kwa sasa na amethibitisha hili kwa kutoa mchango mkubwa uliowawezesha timu ya taifa ya Uingereza kufuzu katika 16 bora ya mashindano EURO 2020

Grealish mwenye umri wa miaka 25 bado yupo kwenye mkataba wa miaka 4 zaidi ndani ya Aston Villa ndiye atakuwa mchezaji ghali zaidi ndani ya EPL iwapo dili lake litakamilika.

Baadhi ya wachezaji waliohamishwa kwa fedha nyingi kwenye ligi ya EPL ni Paulo Pogba 2016 akitokea Juventus kwenda United kwa Bilioni 270 za kitanzania, Harry Maguire Bilioni 240 za kitanzania kutoka Leicester City alipojiunga na Manchester United mwaka 2019.

Wengine ni Romelu Lukaku aliyostimu Manchester United Bilioni 215 za kitanzania alipojiunga nayo akitokea Everton, Virgil Van Djik aliigharimu Liverpool kitita cha Bilioni 215 alipojiunga nao akitokea Southampton 2018 na Kai Havertz aliigharimu Chelsea Bilioni 216 alipojiunga nao akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2020.