
Picha ya moja kati ya mechi iliyowakutanisha Simba na Yanga.
Kupitia taarifa iliyotoa timu hiyo kwa umma imesema kuwa wao watapeleka timu uwanjani saa 11 jioni kama ilivyokuwa awali na kuitaka Bodi ya Ligi kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni ambazo zinawataka kubadili ratiba saa 24 kabla ya mchezo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.
TFF imesema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.