
Carlo Ancelotti na Kaka
Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Brazil, Ancelotti anamtaka Kaká ili kuongeza nguvu katika benchi lake la ufundi hatua itakayowakutanisha tena wawili hawa waliowahi kutamba kwa mafanikio makubwa.
Kaká na Ancelotti waliandika historia ya pamoja ya kuchukua UEFA Champions League msimu wa mwaka (2006/07), Ubingwa wa ligi Serie A (2003/04) wakiwa na AC Milan Kachukua UEFA Super Cup (2003, 2007) pamoja na FIFA Club World Cup (2007)Wakati wanafanya kazi pamoja ndani ya klabu ya AC Milan walifanikiwa kuipandisha katika kileleni cha ubora Barani ulaya.
Kinachosubiriwa kwa hamu ni kwa namna gani wataifikisha timu ya taifa ya Brazil kwenye kilele cha ubora endapo dili hili likifanikiwa.