
Kikosi cha Manchester City
Manchester United atakuwa mwenyeji wa Liverpool pale Old Trafford, matokeo ya sare au ushindi kwa Liverpool yatawafanya ,Manchester City atatangazwa kuwa bingwa wa msimu huu wa 2020-2021wakiwa wameketi majumbani.
Manchester City ana alama 80 baada ya michezo 34 huku United akiwa na alama 67 katika michezo 33. ikiwa ndiyo timu pekee inayoweza kuzifikia alama hizo na kuzipita endapo itashinda michezo yake yote mitano iliyobaki .
Kusare au kufungwa kwa United katika mchezo wa leo, kunatoa maana kuwa hawataweza kutwaa ubingwa hata kama wataishia alama 80 alizonazo City kutokana na idadi tofauti ya magoli yake ya kufunga na kufungwa kuwa mengi , hadi sasa City anampita United magoli 18
Kwa upande wa Italy mazingira yanafanana, endapo Atalanta atafungwa au kusare na Sassuolo kutawafanya Inter Milan kutangazwa mabingwa wapya, Inter ana alama 82 katika michezo 34 zinazoweza kufikiwa na Atalanta pekee mwenye alama 68 katika michezo 33
Endapo Inter atatwaa ubingwa itakuwa mwisho wa utawala wa Juventus iliyochukua ubingwa mfululizo kwa misimu 9, Inter kwa mara ya mwisho ilitwaa ubingwa msimu wa 2009/2010 chini ya Jose Mourinho