Ijumaa , 30th Apr , 2021

Shaka Hamdu Shaka amechukua nafasi ya Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kuanzia leo Aprili 30, 2021. 

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Shaka Hamdu Shaka

Shaka ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro amepitishwa na Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho, baada ya kupendekezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wa Polepole ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge, amewashukuru wanahabari na makundi yote wakiwemo wasanii kwa ushirikiano waliompatia wakati wa uongozi wake.