Ijumaa , 30th Apr , 2021

Mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavani amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa nusu fainali kwenye mashindano makubwa ya vilabau barani ulaya tangu msimu wa 2004-05.

Edinson Cavani

Cavani alifunga mabao mawili jana usiku kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya UEFA Europ League ambapo Manchester United ilikuwa ikicheza dhidi ya AS Roma ya Italia, mchezo ambao Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 6 – 2.

Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay amefunga mabao haya mawili akiwa na Umri wa miaka 34 na siku 74 na kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kufunga mabao mawili kwenye hatua hii tangu alivyo fanya hivyo mchezaji wa zamani wa PSV Philip Cocu ambaye alifunga mabao 2 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa ulaya kati ya PSV na AC Milan akiwa na umri wa miaka 34 na siku 187.

Sasa mshambuliaji huyo anafikisha mabao 12 msimu huu kwenye mashindano yote katika michezo 33 aliyocheza mpaka hivi sasa. cavani alijiunga Manchester United mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya PSG ya Ufaransa.