Ijumaa , 30th Apr , 2021

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili utakaoendelea kumuweka klabuni hadi mwaka 2023.

Mlinzi wa kulia wa Klabu ya Simba, Shomari Kapombe mara baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia msimbazi.

Kapombe ni miongoni mwa wachezaji ambao tangu waliposajiliwa mwaka 2017 wamefanikisha kutwaa ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo huku tukielekea kuchukua kwa mara ya nne.

Uongozi wa klabu chini ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez unaendelea na harakati za kuwaongeza mikataba nyota ambao kandarasi zao zinaelekea ukingoni na bado wanahitajika kwenye timu.

Juzi, Nahodha wa timu, John Bocco aliongeza mkataba na msaizidi wake Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior.’