Alhamisi , 29th Apr , 2021

Bondia wa uzani wa juu, Tyson Fury amesema iwapo mshindani wake Anthony Joshua atapita raundi ya tatu kwenye pambano lao la uzito wa juu basi yeye ataondoka ulingoni na kuacha pambano hilo.

Bondia Tyson Fury (kushoto) na Anthony Joshua (kulia).

Tarehe na eneo la litakalo fanyika pambano lao linazidi kukaribia, na ripoti za hivi laribuni zinadai kwamba Saudi Arabia italipa pauni milioni 108 ili kuipeleka nchini kwao vita hiyo ya mabondia wawili bora kabisa wa Uingereza.

Fury mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akiendeleza majigambo yake kwenye ukurasa wake wa Instagram wiki hii, akimwita tena Antony Joshua wakati akifanya dhihaka hizo katika kuongeza chachu ya mchakato wa pambano lao.

Vilevile alithibitisha mapema wiki hii kuwa mkataba wa kwanza wa mapambano yao mawili kati yake na Joshua utafanyika kati ya Julai 24 na 31 tarehe ambazo zilichaguliwa tangu hapo awali. 

Joshua amepoteza pambano moja tu katika maisha yake ya ngumi dhidi ya Andy Ruiz Jr raundi ya saba ya pambano lao la mwaka 2019.