
Mlinzi wa kulia wa Real Madrid, Dani Carvajal (kushoto) na nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos (kulia).
Carvajal amabye hakufanya mazoezi ya pamoja na Real Madrid tokea jana, alipata maumivu hayo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Chelsea ulioisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Alfredo Di Stefano nchini Hispania.
Tokea kuanza kwa msimu huu, Carvajal amefanikiwa kucheza michezo 15 pekee kutokana na kuandamwa na majerha ya misuli jambo ambalo limeendelea kumsumbua kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande mwingine, Nae nahodha na mlinzi mkongwe wa klabu hiyo, Sergio Ramos amerejea kwenye kambi ya mazoezi ya klabu hiyo na kufanya mazoezi ya pamoja na timu akijiandaa na mchezo dhidi ya Osasuna kesho kutwa kabla ya kurudiana na Chelsea nchini England.
Ramos alikosekana kwa takribani mwezi mmoja kutokana na maumivu ya misuli akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania.