
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo.
ili kutatua changamoto zinazojitokeza.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo wakati akizungumza na EATV ambapo amesema kuwa kwa sasa wanahakikisha wanaondoa changamoto na kero zilizokuwa zikiwakuta walipa kodi nchini kama ambavyo aliagiza Rais katika maagizo yake kwa Mamlaka hiyo.
"Tunatoa Elimu kwa mlipa kodi mlango kwa mlango na tumeanza katika mikoa ya kikodi Temeke, Ilala na Kilimanjaro lengo likiwa ni kuwa karibu na walipa kodi ili watueleze changamoto wanazokutana nazo", amesema Kayombo.
Aidha ameitaja mikoa ambayo tayari imeanza zoezi la mlango kwa mlango kuwa ni mikoa ya kikodi Temeke, Ilala, na Kilimanjaro ambapo lengo ni kuwaweka karibu zaidi walipa kodi.