Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal.
DKT.Bilal amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kilimo ikiwa ni pamoja na katika uzalishaji pamoja na kutafuta masoko ya uhakika ili kuongeza pato kutokana na kilimo.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha nchini Bi. Sadah Mkuya amesema Serikali imeweka utaratibu wa kukutanana na Taasisi za Fedha mara kwa mara ili kutafuta njia ya kuweza kutatua changamoto hizo na Pia ipo katika hatua za Mwisho za kuanzisha benki za Wakulima.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Banki za CRDB Dkt. Charles Kimei amesema njia mojawapo ya kuwajengea wakulima uwezo wa kukopa ni serikali kuangalia upya utaratibu wa kuingiza biadhaa za kilimo kutoka nje.