Ijumaa , 9th Oct , 2020

Golikipa Edouard Mendy aliyesajiliwa katika klabu ya Chelsea majira ya joto yaliyopita atarejea Jijini London kufanyiwa vipimo kugundua ukubwa wa majeraha ya paja lake la kulia.

Golikipa wa Chelsea, Edouard Mendy (Pichani) akiwa mazoezini na timu yake .

Mendy amebeba matumaini ya Frank Lampard kwenye jitihada za kocha huyo kupigania ubingwa wa EPL na hii ni kufuatia Kepa Arrizabalaga kuwa na muendelezo wa kufanya makosa ambayo yalikua yakiigharimu timu hiyo yenye maskani yake Stanford Bridge.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ameaumia mazeozini akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kinachojiandaa kukabiliana na Morroco siku ya Ijumaa na Mauritania Jumanne ijayo.

Taarifa kutoka shirikisho la soka nchini Senegal, zimethibitisha golikipa huyo wa zamani wa Rennes ya Ufaransa kujitoa katika kambi ya timu hiyo baada ya vipimo vya hospitali kuonyesha amepata jeraha katika paja lake la kulia.

Kikosi cha kocha Frank Lampard, kinatarajiwa kurejea uwanjani dhidi ya Southampton Stamford Bridge Oktoba 17 akiwa na mtihani wa kuchagua nani aanze golini kati ya Kepa Arrizabalaga au Willy Caballero.