Alhamisi , 8th Oct , 2020

Nahodha wa Arsenal Pierre Emerick Aubameyang amejiondoa katika timu ya Taifa ya Gabon,sababu kubwa ikiwa ni maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo wa Sheffield Utd jumapili iliyopita.

Pierre Emarick Aubameyang akisahngilia moja ya magoli aliyowafungia Arsenal

Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Taifa ya Gabon Patrice Neveu amesema “ Aubameyang hata kuwa sehemu ya timu katika mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Benin, kama kocha nasikitika kumkosa mchezaji huyu kikosin lakini hamna jinsi''

Aubameyang hajasafiri na timu kuelekea Lisbon nchini Ureno, madaktari wa timu wamethibitisha hawezi kucheza kwa sasa, kwa kuwa mechi hiyo itachezwa jumapili tarehe 11/20/2020,

Kwa upande wa klabu yake ya Arsenal, watakutana na changamoto iwapo watamkosa katika mechi ngumu ijayo dhidi ya Man city tarehe 17/10/2020