
Kituo cha Mabasi Kawe
Wakizungumza na EATV leo abiria na madereva hao wamedai kwamba hata huduma muhimu kama choo haipatilkani ndani ya kituo na hivyo kulazimika kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya jirani kwa kulipia ushuru wa shilingi mia tatu kwa haja ndogo
“Tunalipa kila siku ushuru wa shilingi elfu moja kwa kila daladala linaloingia kituoni hapo lakini tunashangaa hawaboreshi miundombinu ya kituo” amesema Athumani Rajabu dereva wa daladala
Wamesema hicho ni kilio chao cha muda mrefu cha kuililia serikali iwasaidie katika hilo na wamekuwa wakiahidiwa lakini mpaka sasa utekelezaji wake bado na kila siku kinazidi kuharibika hususani kipindi cha mvua