Jumatatu , 5th Oct , 2020

Klabu ya Azam imerejea kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kushinda mchezo wake wa tano mfululizo kwa kuichapa Kagera Sugar bao 4-2 huku mshambuliaji wake Prince Dube akiendeleza kucheka na nyavu katika msimu huu.

Prince Dube ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam Fc na hadi sasa ndiye kinara wa kupachika mabao wa VPL

Azam wamefikisha alama 15 na kukaa kileleni kwa kuvipiku klabu ,za Simba na Yanga wenye alama 13 kila mmoja baada ya kuteremka dimbani mara tano. 

Mshambuliaji wa Azam Prince Dube alifunga Mabao mawili pekeyake huku akitoa Pasi Moja kwa Obrey Chirwa na jingine liliwekwa kimiani na Richard Djold.

Dube anashikilia usukani wa Kupachika mabao ikiwa ndio msimu wake wa Kwanza katika VPL,kafunga mabao matano na pasi za usaidizi wa mabao mbili.

Mchezaji anayemfuatia Dube kwa kupachika mabao ni Meddie Kagere wa Simba ambaye jana aliifungia mabao mawili Simba walipoichapa JKT Tanzania bao 4-0, na sasa mnyarwanda huyo amefikisha  bao 4 hadi katika ligi kuu ya Tanzania bara.