
Wanariadha walioingia tatu bora, Shura Kitata, Vincent Kipchumba na Sisay Lemma
Kitata ameondoka na medali ya dhahabu baada ya kutumia muda wa Saa 02:05:41.
Nafasi ya pili imeshikwa na Vincent Kipchumba wa Kenya ambaye ametumia muda wa 02:05:42.
Ilikuwa siku nzuri kwa taifa za Ethiopia baada ya mwanariadha mwingine kutoka nchi hiyo Sisay Lemma, kumaliza wa tatu akitumia 02:05:45.
Eliud Kipchoge
Eliud Kipchoge amemaliza wa 8 ambapo ameeleza kuwa baada ya kilometa 25 alipata maumivu ya sikio lake la kulia na zikiwa zimebaki kilometa 15 kumaliza akapata maumivu ya nyonga hivyo kupunguza kasi yake.