Jumapili , 4th Oct , 2020

Chama cha Upinzani cha ACT-Wazalendo kimezindua rasmi ilani yake ya uchaguzi visiwani Zanzibar, ambayo imebeba yale wanayotarajia kuyatekeleza kwa wananchi endapo wakipata dhamana ya kuongoza visiwa hivyo.

Uzinduzi wa Ilani ya ACT Wazalendo Zanzibar

Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba 4, katika Hoteli ya Verde visiwani Zanzibar, ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Hamad ambaye pia ni mgombea wa Urais kupitia chama ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani amesema kuwa, inalenga kufungua uchumi wa Zanzibar ambao utawezesha huduma mbalimbali kupatikana kwa urahisi na kuifanya Zanzibar kuwa yenye furaha na raha.

Uzinduzi huo wa kampeni unakuja muda ambao tayari mgombea wa Urais kwa chama hicho ameshaanza kampeni zake visiwani humo akiendelea kunadi sera za chama ambazo zimeorodheshwa kwenye ilani hiyo

Ikumbukwe kuwa chama cha ACT- Wazalendo kilizindua ilani yake ya uchaguzi kwa upande wa Tanzania bara mnamo 31/08/2020 huku Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe akiwa mgeni rasmi.