Jumapili , 4th Oct , 2020

Jana Oktoba 3, 2020 Kamati Kuu ya Chama ya CHADEMA ilifanya kikao Maalum jijini Dar es Salaam, ambacho kilimalizika usiku na kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene, maazimio yatatangazwa leo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe

Makene amechapisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameeleza kuwa maazimio hayo yatatangazwa na Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe.

''Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe leo Jumapili, Oktoba 4, 2020, Saa 7:00 mchana atatoa tamko, kupitia Mkutano wa Waandishi wa Habari, kuhusu maazimio ya Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Chama kilichoketi jana na kumalizika usiku jijini Dar es Salaam'', ameandika Makene.

Hata hivyo Kamati hiyo bado haijawekwa wazi juu ya nini haswa kilijadiliwa kwenye kikao hicho, hali inayofanya watu wengi wasubiri kujua maazimio hususani baada ya mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu, kusimamishwa kufanya kampeni kwa siku saba na Kamati ya Maadili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).