
Msanii Amber Lulu akiwa amepigiwa magoti na Rasco Sembo
Akizungumzia suala hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Rasco Sembo amesema kilichoendelea baada ya pale ni Amber Lulu kumkubali lakini kwa upande wake muda ulikuwa umeshaenda hivyo akaamua kuachana naye.
"Kilichoendelea baada ya pale ni alinikubalia ila muda ulikuwa umeshaenda tayari kwa sababu nilikuwa nishapata pisi kali kutoka Kenya ambapo tupo kwenye mahusiano hivyo nikashindwa kumiliki vitu viwili, Amber Lulu alikua kunikubalia baada ya miezi mitatu, niliamua kumpigia magoti ili aone kama kweli nampenda na kumuaminisha kwa watu" amesema Rasco Sembo
Rasco Sembo alifanya tukio hilo kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV, ambapo Amber Lulu hakumjibu kitu chochote kisha kumuacha na kuondoka akiwa bado amepiga magoti.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.