Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu
Lissu amesema hayo leo Septemba 16 akiwa anazungumza na wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya, juu ya changamoto za wafanyabiasahara wadogo kwa wakubwa ambapo amesema kuwa huo ni mkutano wake wa kwanza na wilayani humo.
"Siku mmechagua rais wa CHADEMA itakuwa ndiyo siku ya mwisho kulipa vitambulisho vya machinga " alisema Tundu Lissu
Aidha Lissu amesema kuwa anataka ukanda unaopakana na nchi jirani kuwa ukanda maalumu wa kiuchumi hivyo serikali yake itakapoingia madarakani hilo ni moja kati ya mambo ambayo watayafanya katika kipindi cha miaka mitano.
"Tunataka ukanda huu unaopakana na Malawi, Zambia, Congo, Rwanda, Burundi, Kenya uwe ukanda maalumu wa kiuchumi" alisema Tundu Lissu.